RONALDO AIBEBA URENO

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliifungia timu yake ya taifa bao pekee katika mpambano dhidi ya Sweden kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika 2014 hapo jana. Ronaldo alifunga katika dakika ya 82 ya mchezo na kuwapa Ureno matumaini ya kuwepo Brazil Juni mwaka ujao. Hata hivyo timu hizo mbili zitasubiri mechi ya marudiano hapo Jumanne ili kufahamu ni timu gani itaungana na Hispania, Uingereza, Bosnia na timu zingine ambazo zimeshakata tiketi ya kushiriki kombe la dunia hapo mwakani.

WACHEZAJI WA UKRAINE WAKISHANGILIA
Katika mechi nyingine, timu ya taifa ya Ufaransa licha ya kuwa na nyota kama Franc Ribery ilishindwa kutamba mbele ya Ukraine baada ya kufungwa 2-0 katika mechi iliyochezwa nchini Ukraine. Roman Zozulya na Andriy Yarmolenko ndio walikuwa mashujaa wa Ukraine ambao watasubiri mechi ya marudiano kujua hatma yao. Beki Mfaransa anayeichezea Arsenal ya Uingereza, Laurent Koscienly alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 91 huku dakika tano baadae mchezaji wa Ukraine Kucher nae akioneshwa kadi nyingine.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates