Home Unlabelled FEZA AIAGA THE CHASE
FEZA AIAGA THE CHASE
By burudanibuzz At August 11, 2013 0
Feza Kessy, mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother ameondolewa mjengoni hapo jana baada ya kukaa ndani ya jumba la Big Brother kwa wiki 20. Kutolewa kwa Mtanzania huyo ambaye pia ni msanii wa muziki na mwanahabari kunamaanisha Tanzania haina mwakilishi mwingine baada ya Nando kutolewa takribani wiki mbili zilizopita. Feza ameondoka huku watu mbalimbali barani Afrika wakisubiri kuona kama penzi lake na mshiriki kutoka Botswana O'neal litaendelea. Kama Feza na O'neal wataendeleza mahusiano yao wataungana na Kevin & Elizabeth pamoja na Mwisho na Meryl ambao walianzisha mahusiano baada ya kukutana BBA.