ALBAMU YA SELENA YAKIMBIZA SOKONI

Mwanamuziki na muigizaji Selena Gomez kwa mara ya kwanza amefanikiwa kupanda na kushika nafasi ya kwanza kwa mauzo ya albamu katika
Billboard hot 200. Albamu ya Selena inayoitwa Stars Dance imeuza nakala 97,000 katika wiki yake ya kwanza. Hii ni albamu ya kwanza ambayo Selena ameshiriki kushika nafasi ya kwanza huku mafanikio yake mengine ni katika albamu ya kundi lake la Selena Gomez & The Scene ambapo albamu ya When the sun goes down ilifika nafasi ya tatu. Kiss and Tell na A year without rain ni albamu zingine ambazo mwanadada Selena ameshiriki.
Albamu ya sasa STARS DANCE ina jumla ya nyimbo 13. Wimbo Come n get it ulikua wa kwanza kutolewa katika albamu hiyo ilifika nafasi ya sita kwenye Billboard 100.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates