ROONEY

Huku vuguvugu la usajili barani ulaya likiendelea, taarifa zisizo rasmi zinaeleza kuwa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Mark Rooney yuko mbioni kujiunga na timu ya Chelsea "The Blues". Rooney ambaye amekuwa kwenye mgogoro na klabu yake kuhusu suala la uhamisho inasemekana anaweza kwenda Chelsea kwa paundi milioni 28.9. Timu ya Arsenal nayo imeongeza juhudi zake kumnasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 27. Taarifa za ndani zinadai kuwa Rooney tayari amekubaliana na mshahara wa Paundi 220,000 na Chelsea katika mazungumzo ya siri.
Kwa mujibu wa Dailystar, Manchester wanamwachia Rooney ili waongeze pesa kwa ajili ya kumnyakua kiungo wa Barcelona Francesc Fabregas.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates