Gerardo Martino ametangazwa kuwa kocha mpya wa Barcelona kuchukua nafasi ya Tito Vilanova aliyeacha mikoba ya kuino timu hiyo wiki iliyopita. Martino alikuwa kocha wa timu iliyomtoa Lionel Messi Newell's Old Boys nchini Argentina. Kocha huyo mpya wa Barc hana mafanikio sana kwenye soka hasa la kimataifa baada ya kuifundisha timu ya taifa ya Paraguay kwa muda. Martino ambaye enzi zake uwanjani alikuwa anacheza kama kiungo mshambuliaji nakabiliwa na changamoto ya kurudisha makali na heshima ya Barcelona ambayo kwa msimu uliopita umeporomoka.
Martino atasaini mkataba wa miaka mitatu kukaa Camp Nou