KWA HERI FERGUSON- MAN UNITED











Timu inayobeba rekodi ya kuwa mabingwa mara nyingi kwenye ligi kuu ya Uingereza na mabingwa wa msimu wa 2012/2013 Manchester United wamethibitisha taarifa za kocha wao Sir. Alex Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu huu. Mechi kati ya Manchester United na West Bromwich Albion itakayochezwa May 19 ndiyo itakuwa ya mwisho kwa kocha huyo mwenye historia nzuri na Man U. Sir Alex Ferguson amekaa United kwa miaka 27 na kufanikiwa kuondoa ubabe wa Liverpool huku Mzee huyo akifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu mara 13 tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 1986. Mara baada ya kuthibitika kujiuzulu kwake kocha waEverton David Moyes ni mmoja kati ya wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo akiwa na sapoti ya kipa wa zamani wa Manchester United Mdenmark Peter Schmeichel. Schmeichel akimzungumzia Moyes amesema"David Moyes has been more than a decade at Everton on limited funds and he's been doing a fantastic job. He's Scottish, he's made from the same cloth as Sir Alex.".
Kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho pia ametajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaoweza kupewa nafasi hiyo. Ferguson mwenyewe amewahi kukaririwa akisema kwamba angependa Jose Mourinho aiongoze Man U baada ya yeye kuachia nafasi hiyo. Mourinho ana hatihati ya kubaki Real Madrid lakini kocha huyo pia anahitajika na timu yake ya zamani Chelsea.

Vikombe alivyofanikiwa kunyakua akiwa United-

Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates