ANGELINA JOLIE AKATWA MAZIWA




Mwigizaji nyota Hollywood Angelina ameamua kukatwa maziwa yote mawili (Mastectomy). Mwanamama huyo ametangaza hayo kama hatua za mwanzo ili kumkinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya matiti iliyokuwa inatishia afya yake. Angelina Jolie ambaye ni mchumba wa mwigizaji Brad Pit wana watoto sita huku watatu wakiwa wa kuasiliwa (Adopted). Mama wa mwigizaji huyo alifariki kwa ugonjwa wa saratani ya matiti na Angelina aligundulika kuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo. Angelina mwenye miaka 37 ametolewa kizazi kutokana na uwezekano wa kupata saratani ya kizazi.Angelia ameigiza muvi nyingi huku zilizokimbiza zaidi ni pamoja na Salt, Original sin, Changeling, The Bone Collector, A mighty Heart pamoja na Mr & Mrs Smith
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates