PEDRO AKISHANGILIA |
Timu inayosemekana kuwa bora duniani kwa sasa Barcelona ikiwa nyumbani Nou Camp jana ilitoka sare ya 1-1 na Paris Saint Germain na kusonga mbele hadi hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya (UEFA). Barca ambao walipata sare nyingine ya 2-2 walipocheza mechi ya kwanza nchini Ufaransa hivyo matokeo ya jana yameifanya Barca kusonga mbele kutokana na magoli mawili ya ugenini. Lionel Messi alilazimika kucheza kipindi cha pili licha ya kuripotiwa kuwa na maumivu ya misuli aliyopata kwenye mechi ya kwanza dhidi ya PSG. Javier Pastore aliifungia PSg bao la kuongoza dakika ya 50 kabla ya Pedro kusawazisha dakika ya 72.
Katika mechi nyingine Bayern Munich waliiaibisha Juventus baada ya kushinda 2-0 nchini Italia na hivyo kuitoa Juve kwa jumla ya mabao 4-0. Mario Mandzukic na Claudio Pizzaro ndio walikuwa mashujaa wa Bayern wakiwaacha Juve na aibu ya kufungwa mechi zote mbili. Bayern walipata ushindi wa 2-0 timu hizo zilipokutana